‘Ahh’ yazidi kumpaisha Herman Zimbabwe

0
71

HARARE, ZIMBABWE

MSANII wa kizazi kipya anayefanya vyema Zimbabwe, Herman, ametamba kuwa ngoma yake mpya, Ahh, imezidi kumtambulisha ndani na nje ya nchi hiyo.

Herman mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ameiambia mtanzania.co.tz kuwa wimbo ‘Ahh’ umepokewa vizuri kwenye platforms zote ya kusikiliza na kupakua muziki duniani.

“Wimbo wangu unaitwa Ahh maana yake ni I Love You, nimeitoa siku mbili hizi lakini nashukuru fanbase yangu imewezesha niwe na ‘streams’ nyingi kwenye mitandao yote ya kusikiliza na kupakuwa muziki namba zangu ni kubwa lakini bado nahitaji sapoti ili nizidi kufanya vizuri zaidi hapa Afrika,, video imeshatoka hivyo naomba mashabiki waingia YouTube chaneli ya Herman kuitazama naamini wataburudika,” amesema Herman.

Source: mtanzania.co.tz