Mapokezi Yanga ni shangwe Kigoma

0
42

Na Winfrida Mtoi

Kikosi cha Yanga kimetua mkoani Kigoma asubuhi ya leo Alhamisi na kupata mapokezi ya aina yake kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.

Wanajangwani hao wamewasili mkoani humo kwa maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya watani wao Simba utakaochezwa Jumapili Julai 25,2021.

Mashabiki na wadau wa Yanga, Kigoma wamejitokeza kwa wingi kuipokea timu yao, huku wakitamba kuwa mtani wao hataondoka na kitu.

Yanga itakutana na Simba ambayo wametoka kuifunga katika mchezo wa Ligi  Kuu Bara, ulichezwa Julai 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Source: mtanzania.co.tz